TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUTOKEA KWA TETEMEKO LA ARDHI KATIKA MKOA KATAVI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUTOKEA KWA TETEMEKO LA ARDHI KATIKA MKOA KATAVI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MADINI
TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA (GST)
Mnamo tarehe 9/09/2019 majira ya saa 9:38 usiku kumetokea tetemeko la ardhi katika kijiji cha Sibwesa Kata ya Sibwesa karibu na ziwa Tanganyika katika mkoa wa Katavi Wilayani Mpanda DC (Wilaya ya Tanganyika). Taarifa zilizokusanywa na kuchakatwa kutoka kwenye kituo cha kuratibu matetemeko ya ardhi kilichopo Dodoma katika ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), zinaonesha kuwa tetemeko hilo lina ukubwa wa 5.5 katika kipimo cha Ritcher. Kitovu cha tetemeko hilo  kipo umbali wa kilometa 35.5 Kusini– Magharibi ya mji wa Mpanda kwenye latitude 6.47°S na longitude 30.77°E.  Eneo hili lipo katika ukanda wa bonde la ufa la Afrika Mashariki, mkondo wa Magharibi ambao ni njia kubwa ya matetemeko ya ardhi. Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mashuhuda mbalimbali, tetemeko hili limesikika katika maeneo ya miji ya Mpanda, Mpanda DC na Sumbawanga, Ukubwa wa tetemeko h... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More