Taarifa Kwa Umma Kuhusu Takwimu Za Deni La Serikali Kwa Benki Kuu Ya Tanzania - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Takwimu Za Deni La Serikali Kwa Benki Kuu Ya TanzaniaBenki kuu ya Tanzania (BoT) inakanusha taarifa potofu zinazozosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa Benki Kuu imechapisha noti zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya matumizi ya serikali.
Benki Kuu inauarifu Umma kuwa, taarifa hiyo sio sahihi na inalenga kuathiri imani ya Wananchi na wadau wa kimataifa kuhusu uthabiti wa fedha ya Tanzania. Aidha, Benki Kuu inawaasa Wananchi kuwa utoaji wa taarifa potofu kuhusu sekta ya fedha unaweza kuleta athari kubwa kwa mwenendo wa uchumi. Hivyo ni vyema Wananchi wajue yafuatayo kuhusu utoaji wa fedha kwa matumizi ya Serikali:
1.Mapato ya serikali hayawiani moja kwa moja na matumizi yake mwezi-hadi-mwezi. Kuna wakati mapato yanakuwa makubwa mfano miezi ya mwisho wa robo mwaka na wakati mwingine yanakuwa madogo. Kwa sababu ya kupishana kwa mapato na matumizi ya serikali, sheria imeruhusu serikali kuchukua mkopo wa muda mfupi kutoka Benki Kuu ili kuziba pengo pale linapotokea na kurejesha baadaye. Utaratibu huu unat... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More