TAARIFA KWA WAOMBAJI MIKOPO KUSAHIHISHA TAARIFA ZAO - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAARIFA KWA WAOMBAJI MIKOPO KUSAHIHISHA TAARIFA ZAOMAREKEBISHO YA TAARIFA KWENYE MAOMBI YA MIKOPO HESLBBodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 na umma kwa ujumla kwamba imetangaza orodha ya baadhi ya waombaji mikopo ambao fomu zao za maombi ya mikopo zina upungufu ili waweze kufanya marekebisho kwa njia ya mtandao https://olas.heslb.go.tzkwa siku saba (7) kuanzia Jumatatu  Septemba 24 hadi Jumapili  Septemba 30, 2018.


Katika kipindi hicho waombaji wote wa mikopo ambao fomu zao zina upungufu wa baadhi ya taarifa na nyaraka zao ama za wadhamimi wao, watapaswa kusoma majina yao kwenye orodha iliyowekwa kwenye tovuti ya HESLB www.heslb.go.tz na kisha kuingia kwenye mtandao wa maombi ya mikopo ili kufanya masahihisho kwa kufuata hatua zilizowekwa na baada kukamilisha, waziwasilishe ndani ya muda uliopangwa bila kutuma kwa njia ya EMS.


Nyaraka zote zinazokosekana ikiwa ni pamoja na vyeti vya kuzaliwa au vya vifo vya wazazi, kurasa za taarifa na saini za mwombaji n... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More