TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MBEYA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MBEYA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu watatu kwa tuhuma mbalimbali.

KUINGIA NCHINI BILA KIBALI,
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 16:30 jioni huko eneo na Kata ya Lupa Tingatinga, Tarafa ya Kipambawe. Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Polisi walimkamata OMARY JUMA @MWAMI [21] raia wa nchi ya Burundi akiwa ameingia nchini bila kibali na kufanya shughuli za kilimo cha Tumbaku. Upelelezi unaendelea.

UNYANG’ANYI WA KUTUMIA NGUVU
Mnamo tarehe 21.03.2019 saa 00:30 usiku huko maeneo ya Veta Kata ya Ilemi, Tarafa ya Iyunga ndani ya Jiji na Mkoa wa Mbeya. IMAN ANDISON [20] Dereva bodaboda na mkazi wa Simike alinyang’anywa pikipiki yake yenye namba za usajili MC 833 BVS aina ya Kinglion na watu watatu wasiofahamika.
Mbinu iliyotumika ni kwamba muhanga akiwa amepaki pikipiki yake maeneo ya Kiwira Motel alitokea abiria mmoja na kutaka apelekwe Veta na ndipo alipomfikisha maeneo hayo walijitokeza watu wengine wawili na kumvamia kisha kumjeruhi kichwani na watu hao kutokomea ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More