TAARIFA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAARIFA ZA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEOJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za makosa mbalimbali.


MAUAJI

Mnamo tarehe 13.03.2019 majira ya saa 13:30 mchana huko Kitongoji cha Igadu, Kijiji cha Shuwa, Kata ya Iyunga – Mapinduzi, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. TAMKA D/O MAMBA @ NGANGALE [28] Mkazi wa Kitongoji cha Masanga “A” aligundua kuuawa kwa mume wake aitwaye HADSON S/O HAIWOLE MWANGOKA [45] Mkazi wa Masanga “A” na mtu/watu wasiofahamika.


Marehemu aliondoka nyumbani tarehe 11.03.2019 saa 05:00 alfajiri kwenda shambani Kitongoji cha Igadu na hakurudi tena, harakati za kumtafuta zikaanza wakiwa wanamtafuta maeneo ya shambani kwenye korongo ndipo waliona kiganja cha mkono wa kulia kikiashiria kuna mwili wa marehemu umefukiwa.


Polisi walifika eneo la tukio na kukuta kiganja cha mkono korongoni na baada ya kufukua ulikutwa mwili wa marehemu aliyetambuliwa kuwa ni HADSON HAIWOLE MWANGOKA huku ukionekana kupigwa kitu kizito usoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More