Taarifa za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Salah, Sarri, Lampard, Foyth, Rabiot na wengine sokoni - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taarifa za usajili barani Ulaya Jumanne hii, Salah, Sarri, Lampard, Foyth, Rabiot na wengine sokoni

Juventus wanajipanga kutoa kitita cha pauni milioni 175 ili kumsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 26. (Sky Arabia – via 90min) Mustakabali wa Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo. (Telegraph)

Wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha ‘kurekebishana’ katika uwana wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kufuatia kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)

Kocha wa Derby Frank Lampard amepuuzia uvumi kuwa huenda akarithi mikoba ya Maurizio Sarri endapo Chelsea itaamua kumfukuza. (Evening Standard). Beki wa Tottenham Juan Foyth, 21, amefichua kuwa alikataa kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain tili ajiunge na Spurs mwaka 2017. (Goal)

Kocha wa Chelsea raia wa Italia Maurizio Sarri amekalia kuti kavu baada ya mfululizo wa vipigo kwa timu yake.

Barcelona wamefikia makubaliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili streka wao raia wa Serbia Luka Jovic, 21, mwishoni mwa msimu. (... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More