TAASISI YA AGRI THAMANI FOUNDATION YASAINI MKTABA WA MAKUBALIANO NA OFISI YA MKUU WA MKOA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO YA LISHE KAGERA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAASISI YA AGRI THAMANI FOUNDATION YASAINI MKTABA WA MAKUBALIANO NA OFISI YA MKUU WA MKOA KUTOKOMEZA CHANGAMOTO YA LISHE KAGERA

Na: Sylvester Raphael
Taasisi mpya ya Agri Thamani Foundation iliyoanzishwa kwa lengo kuu la kuboresha lishe Mkoani Kagera na kuongeza ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kuongeza Mnyororo wa thamani kwenye Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetiliana saini na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika Mkataba wa Makubaliano ili kuanza utekelezaji wa shughuli zake ifikapo Novemba Mosi, 2018.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Taasisi ya Agri Thamani Foundation ambaye ni mzawa wa Mkoa wa Kagera Bi Neema Lugangira mara baada ya kutiliana saini kwenye Mkataba wa Makubaliano na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Nesphory Bwana alisema kuwa aliamua kuanzisha Taasisi hiyo kutokana na Mkoa wa Kagera kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye udumavu na utapiamlo kutokana na kutopata lishe bora na stahiki.
“Nimeamua nianzishe Taasisi ambayo itausaidia Mkoa wetu wa Kagera hasa kuondoa udumavu kwa watoto kwani ukiangalia haraka utaona kuwa Mkoa wa Kagera kila zao linakubali kustawi lakini wato... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More