Taasisi ya Dk Mengi kutoa tuzo kwa walemavu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taasisi ya Dk Mengi kutoa tuzo kwa walemavu

Taasisi ya Dr Reginald MENGI ya kusaidia watu Wenye ulemavu imeamua kutoa tuzo kwa Watu Wenye ulemavu ili kuihamasisha jamii kutambua kuwa  watu hao wana uwezo wa kufanya makubwa.Akitangaza utoaji wa tuzo hizo za " I can", jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dr Reginald MENGI Persons with Disabilities, Bi. Shimimana Ntuyabaliwe amesema Tuzo za mafanikio katika maeneo saba tofauti zitatolewa kwa washiriki watakaoshinda baada ya kupitia mchakato wà uteuzi.Amesema tuzo hizo zimewalenga watu wenye ulemavu waliofanikiwa kwenye nyanja za elimu, siasa, uongozi, ujasiriamali, Sanaa na burudani, michezo, na ujuzi wa kipekee na ametaja sifa za watu wanaostahili kuwania tuzo hizo.Amesema washindi watatangazwa na kukabidhiwa tuzo hizo, na fedha taslimu tarehe 2 February mwakani wakati wa tafrija ya kila mwaka  ya chakula cha mchana kwa watu wenye ulemavu inayoandaliwa na Dr Reginald Mengi.Amewataka watu wenye sifa watume mapendekezo yao kwenye Taasisi hiyo kwa njia za barua pep... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More