TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA KIGOMA - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA KIGOMA

Mradi wa Kuwawezesha vijana wa kike na wanawake kiuchumi kupitia Tasnia ya Urembo na Vipodozi ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wamemaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma Yaliofanyika kwa wiki mbili kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yaliyotolewa bure yamewanufainsa wanawake 20 kutoka Mkoani Kigoma na vitongoji vya jirani. Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.
Awamu ya pili walipata ujuzi jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi salama vya LuvTouch Manjano.Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazot... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More