Taasisi ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taasisi ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema

TAASISI isiyo ya kiserikali (NGOs) ya Marafiki Tanzania Charity yazindua siku ya Matendo mema (Good Deeds Day) ambayo kidunia itafanyika Aprili 7,2019.


Siku hii ya matendo mema itahusisha uchangiaji wa vitu mbalimbali pamoja na huduma kwa watu wenye mahitaji katika jamii.


Akizungumza katika uzinduzi wa siku ya matendo mema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira, January Makamba ambaye pia amechaguliwa kuwa mlezi wa Marafiki Tanzania Charity amewaomba wananchi kujiunga na Marafiki Tanzania Charity ili kuweza kufanikisha kuchangia vitu mbalimbali ikiwa pamoja na huduma kwaajili ya wahitaji katika jamii yetu.
Pia Makamba amewaomba wanamarafiki Tanzania Charity kutumia Lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka kwa kila mtanzania ili kuongeza wana marafiki Tanzania kuwa wengi zaidi.
Nae Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi-Sinza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Padre Josephat Mhozya amehamasisha kila mtu kutenda matendo mema.
"Kutenda matendo mem... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More