Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wamshukuru Rais Magufuli. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wamshukuru Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Prof. Mohammed Janabi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuisaidia Taasisi hiyo kupata jengo la Kitengo cha Matibabu ya Moyo kwa Watoto.
Prof. Janabi amefafanua kuwa kufuatia maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli aliyoyatoa mapema mwaka jana (2018), moja ya majengo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili lililopo jirani na Taasisi hiyo lilikabidhiwa kwa Taasisi hiyo na Serikali ikatoa fedha za kulikarabati na kuwekewa miundombinu ya kutolea huduma za matibabu ya moyo kwa watoto.
Ameongeza kuwa jengo hilo lina lina vitanda 40 vya kawaida na vitanda 8 vya watoto wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) na kwamba kukamilika kwake kutaiwezesha Taasisi hiyo kupata vyumba vipya 4 vya kliniki ambavyo vitawawezesha Madaktari kuwaona watoto 60 kwa siku.
Prof. Janabi amebainisha kuwa kabla ya kupatiwa jengo hilo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ililazimika kuwachanganya w... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More