TAASISI YA SADAKA NETWORK,HOSPITALI YA MUHIMBILI,AGA GHAN NA WOMEN TO WOMEN FOUNDATION KURUDISHA TABASAMU USONI KWA WATU WALIOHARIBIKA MAUMBILE YAO. - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAASISI YA SADAKA NETWORK,HOSPITALI YA MUHIMBILI,AGA GHAN NA WOMEN TO WOMEN FOUNDATION KURUDISHA TABASAMU USONI KWA WATU WALIOHARIBIKA MAUMBILE YAO.

Watanzania wameombwa kwa pamoja kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya SADAKA NETWORK , Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan kwa kushirikiana na Women to women foundation kuchangia kurudisha tabasamu usoni  kwa wakina mama na watoto waliopata matatizo hayo kwa  bahati mbaya, kupata ajali,kwa ukatili wa kijinsia, kupigwa au matatizo yoyote yaliyopelekea wao kuharibika maumbile yao ikiwa ni usoni ama sehemu nyengine ya mwili. 
Mwanzilishi wa taasisi hiyo Dkt. Ibrahim Msengi akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa gharama za kuwatibu watoto na akina mama ni kubwa na haziwezi kubebwa na Muhimbili au Aga Ghan peke yake wala Women to women foundation,bali ghalama hizi zitafanikiwa endapo wananchi wataungana kwa pamoja ili kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi hilo.
"Upasuaji huu utafanyika katika Hospitali ya Muhimbili na Aga Ghan na tunatarajia kuwafanyia upasuaji watu 40 kutoka sehemu zote Tanzania,hivyo pesa inayohitajika ni Tsh Milioni 268" alisema Dkt. Msengi.Dkt. Ibrahi... Continue reading ->


Source: Mwanaharakati MzalendoRead More