TADB, TUME YA UMWAGILIAJI WAJIPANGA KUCHAGIZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TADB, TUME YA UMWAGILIAJI WAJIPANGA KUCHAGIZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Katika kutekeleza kwa vitendo jukumu la kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Tume ya Umwagiliaji ya Taifa (NIRC) ili kuchagiza kilimo cha umwagiliaji nchini.
Akizungumza wakati wa utiaji wa saini wa makubaliano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine alisema benki imejipanga kuchagiza tasnia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo.
“Ili kuninua uzalishaji wenye tija katika sekta ya kilimo nchini benki imejipanga kuwekeza mtaji wa kutosha katika kilimo cha umwagiliaji,” alisema.
Bw. Justine aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imeshatoa mkopo katika miradi 9 mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Mhandisi Dkt. Eliakim Matekere alisema tasnia ya umwagiliaji ina mchango mkubwa katika kunyanyua uzalishaji nchini hatahivyo muitikio finyu wa wadau umekuwa ukirudisha nyuma tasnia hiyo.
Mhandisi Dkt. Mate... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More