TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO BAHARI BEACH MAANDALIZI MECHI NA UGANDA MACHI 24 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI KESHO BAHARI BEACH MAANDALIZI MECHI NA UGANDA MACHI 24

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinatarajiwa kuingia kambini kesho katika hoteli ya Bahari Beach iliyopo Kunduchi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baadaye mwezi huu.
Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Uganda, The Cranes Machi 24, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam katika mchezo wa mwisho wa Kundi L kufuzu AFCON Juni 2019 nchini Misri.
Na baada ya kikao cha pili cha Kamati ya Saidia Taifa Stars wiki hii mjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kikosi kinaingia kambini kesho.

Taifa Stars inahitaji ushindi tu katika mchezo huo wa mwisho ili kufuzu AFCON ya pili kihistoria, huku ikiombea matokeo mabaya Lesotho mbele ya Cape Verde mjini Praia katika mchezo mwingine wa mwisho wa Kundi L.
Uganda tayari imejihakikishia kucheza AFCON ya Juni nchini Misri baada ya kufikisha pointi 13, wakati Lesotho inayoshika nafa... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More