TAIFA STARS KUMENYANA NA BURUNDI KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS KUMENYANA NA BURUNDI KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA QATAR 2022

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TANZANIA itamenyana na Burundi katika hatua ya awali kuwania kupangwawa kwenye makundi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotoka leo, mechi ya kwanza baina ya Taifa Stars na Int’hamba Murugamba itachezwa Uwanja wa Taifa mjini Bujumbura Septemba 2 kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 10 mjini Dar es Salaam. 
Mechi nyingine Ethiopia itamenyana na Lesotho, Somalia na Zimbabwe, Eritrea na Namibia, Djibouti na Eswatini, Botswana na Malawi, Gambia na Angola na Liberia dhidi ya Sierra Leone.

Nao Mauritius watamenyana na Msumbiji, Sao Tome na Principe dhidi ya Guinea-Bissau, Sudan Kusini na Equatorial Guinea, Comoro na Togo, Chad na Sudan na Shelisheli dhidi ya Rwanda.
Washindi 14 wa jumla wataungana na timu nyingine 26 za viwango vya juu barani, wakiwemo majirani Kenya na Uganda kugawanywa kwenye makundi 10 ya timu tano kila moja kuanza rasmi kuwania tiketi ya Qatar 2022.
Washindi wa makundi yote wataingia hatua ... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More