TAIFA STARS WAMEONDOKA ALFAJIRI KWENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI KUJIANDAA NA LESOTHO - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS WAMEONDOKA ALFAJIRI KWENDA KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI KUJIANDAA NA LESOTHO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeondoka Alfajiri ya leo kwenda mjini Blomofontein, Afrika Kusini kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho katikati ya mwezi huu kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon.
Taifa Stars watakuwa wageni wa Mamba wa Lesotho Novemba 18, mwaka huu Uwanja wa Setsoto mjini Maseru katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ya mwakani na kuelekea mchezo huo, watakuwa kambini Afrika Kusini kwa siku 10.
Wachezaji waliosafiri na Stars leo pamoja na makipa Aishi Manula wa Simba SC, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya wa Yanga SC na Benedictor Tinocco wa Mtibwa Sugar zote za nyumbani. 
Mabeki ni Shomary Kapombe, Erasto Nyoni wa Simba SC, Ally ‘Sonso’ Abdulkarim wa Lipuli FC, Kelvin Yondan, Gardiel Michael wa Yanga SC, Aggrey Morris na Abdallah Kheri wa Azam FC, zoyte za nyumbani.
Viungo ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya wa Azam FC, Salum K... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More