TAIFA STARS WATOTA PRAIA, WAPIGWA MABAO MAWILI NA MTU MMOJA, WALALA 3-0 KWA CAPE VERDE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS WATOTA PRAIA, WAPIGWA MABAO MAWILI NA MTU MMOJA, WALALA 3-0 KWA CAPE VERDE

Na Mwandishi Wetu, PRAIA
NDOTO za Tanzania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zimeanza kuyeyuka baada ya leo kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, Cape Verde katika mchezo wa Kundi L uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Praia.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa Mali, Boubou Traore, Drissa Kamory Niare na Baba Yomboliba, mabao yaliyoizamisha Taifa Stars leo yamefungwa na mshambuliaji wa klabu ya Partizan ya Ligi Kuu ya Serbia, Ricardo Jorge Pires Gomes na beki wa MOL Vidi FC ya Hungary Ianique dos Santos Tavares maarufu kama Stopira.
Cape Verde inapanda kileleni kwa wastani mzuri wa mabao baada ya kufikisha pointi nne, sawa na Uganda ambao kesho watacheza mechi ya tatu na Leshoto yenye pointi mbili sawa na Tanzania. 

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta leo Uwanja wa Taifa mjini Praia

Huo utakuwa mchezo wa tatu wa Taifa Stars katika kundi bila ushindi, baada ya awali kutoa sare za 1-1 na Lesotho Dar es Salaam na 0-0 na Uganda mjini Kampala.
Kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike akiion... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More