TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA MISRI SALAH NA EL NENY WAKIWA BENCHI ALEXANDRIA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS YACHAPWA 1-0 NA MISRI SALAH NA EL NENY WAKIWA BENCHI ALEXANDRIA

Na Mwandishi Wetu, ALEXANDRIA
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania imechapwa bao 1-0 na wenyeji, Misri katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Bao pekee la wenyeji kwenye mchezo huo maalum kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kuanza Juni 21 hadi Julai 19 nchini Misri limefungwa na kiungo wa Aston Villa ya England, Ahmed El Mohamady dakika ya 64 akimalizia pasi ya beki wa Pyramids ya nyumbani, Ahmed Ayman Mansour.
Pamoja na kufungwa, Taifa Stars inayofundishwa na Mnigeria, Emmanuel Amunike ikiongozwa na Nahodha wake, mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ilicheza vizuri – lakini ukweli tu ilizidiwa na Mafarao.
Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta akimtoka beki wa Misri, Mahmoud Alaa leo  
Mbwana Samatta (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na marefa na Nahodha na mfungaji wa bao la Misri leo, Ahmed El Mohamady (wa pili kushoto) kabla ya mchezo wa leo 

Kocha Mmexico anayeinoa Misri aliwaacha benchi muda wot... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More