TAIFA STARS YAWAFUATA CAPE VERDE BILA MKUDE, DANTE NA DOMAYO…AMUNIKE ABEBA MAKIPA WANNE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAIFA STARS YAWAFUATA CAPE VERDE BILA MKUDE, DANTE NA DOMAYO…AMUNIKE ABEBA MAKIPA WANNE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mnigeria, Emmanuel Amunike ameongeza makipa wawili, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons na Benedicto Tinocco wa Mtibwa Sugar katika kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachoondoka usiku huu kwenda Praia nchini Cape Verde.
Na hao wanaungana na makipa wengine wawili, Aishi Manula wa Simba SC na Beno Kakolanya wa Yanga kwa safari leo, baada ya kuachwa kwa Mohammed Abdulrahman wa JKT Tanzania ambaye ameumia.
Pamoja na Abdulrahman, Amunike pia amewatema beki Andrew Vincent ‘Dante na viungo Jonas Mkude na Frank Domayo kwa sababu wote ni majeruhi, wakati kiungo Salum Kihimbwa na mshambuliaji Kelvin Sabato wameachwa kwa sababu za kiufundi.
Beki Andrew Vincent 'Dante' hatasafiri na Taifa Stars usiku huu kwenda Praia kwa sababu ni majeruhi 

Viungo wengine, Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Farid Mussa na washambuliaji Shaaban Iddi Chilunda wote wa CD Tenerife ya Hispania na Nahodha Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgij... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More