Takriban watu 12 wameuawa akiwemo afisa wa polisi katika kilabu moja ya burudani Oaks, California. - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Takriban watu 12 wameuawa akiwemo afisa wa polisi katika kilabu moja ya burudani Oaks, California.

Takriban watu 200 waliripotiwa kuwa ndani ya kilabu ya Borderline and Grill wakati wa shambulio hilo. Maafisa wanasema mshukiwa huyo alipatikana amefariki ndani ya eneo hilo la burudani na bado hawajamtambua. Hawajui lengo lake la kutekeleza kisa hicho. Sherehe ya muziki wa aina ya country music miongoni mwa wanafunzi ilikuwa ikiendelea wakati mshukiwa huyo ambaye alikuwa amevalia nguo nyeusi, alipoingia katika baa hiyo na kuanza kufyatua risasi. Ripoti zinasema kuwa huenda mshukiwa huyo alitumia maguruneti ya moshi na bunduki inayojulikana kwa jina handgun kulingana na walioshuhudia. Kwa mujibu wa BBC, Mtu mmoja aliyekuwa amejeruhiwa aliambia runinga ya KTLA: Tulilala chini tulisikia watu wakipiga kelele. rafiki yangu ndio DJ hivyobasi alisitisha muziki tulisikia kelele nyingi. Shahidi mwengine , Teylor Whittler, alisema: “Nilikuwa katika sakafu ya kucheza densi na nikasikia milio ya risasi , hivyobasi niliangalia nyuma na mara nikasikia kila mtu akisema laleni chini. “Tulibabai... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More