TAKUKURU JIRIDHISHENI NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI-MAJALIWA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAKUKURU JIRIDHISHENI NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWA WANANCHI-MAJALIWA

 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa TAKUKURU wajiridhishe huduma zinatolewa kwa wananchi bila ya rushwa, watakapobaini rushwa wachukue hatua.
Pia, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wajiepushe na vitendo vya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika utendajikazi wao.
Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa JWTZ.
“Msiwalazimishe au kutengenezea mazingira ya kuomba rushwa kwa wananchi. Wananchi mkiona mnazungushwa katika kupatiwa huduma katoeni taarifa TAKUKURU.”
Waziri Mkuu amesema “tabia ya njoo kesho njoo kesho haikubaliki katika Serikali hii. Serikali haitaki mtumishi mzembe anayedharau wananchi, fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zenu.”
Amesema Rais Dkt. John Magufuli anataka kila Mtanzania afikiwe na huduma za jamii bila ya ubaguzi wa aina yoyote, mtumshi atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake hatakuwa na ... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More