TAKUKURU YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS DK.MAGUFULI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAKUKURU YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS DK.MAGUFULI

*Ni yale aliyoyatoa wakati wa kikao cha wafanyabiashara *Yatangaza kuwafikisha Mahakamani watumishi wa TRA, Polisi *Yapeleka timu kuwachunguza askari walionyanyasa wafanyakazi Moro

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(TAKUKURU)imesema tayari imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli ambayo ameyatoa Juni 7,2019 wakati wa kikao kazi kati yake na wafanyabishara nchini .
Kwa mujibu wa TAKUKURU imesema imeanza kufanyia kazi na kuchukua hatua mbalimbali za uchunguzi kuhusu tuhuma za mfanyabishara aliyeuzuliwa mzigo wake tangu mwaka 2016.
Katika kutekeleza maagizo hayo TAKUKURU leo Juni 10,2019 imesema itawafikisha mahakamani watumishi watatu waliohsika na ukamataji na uzuiaji wa mzigo wa mfanyabiashara Ramadhan Hamisi Ntunzwe kwa makosa ya rushwa.
Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Juni 10 , 2019 amewataja watumishi hao ni Charity Ngalawa muajiriwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Askari... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More