TAMADUNI ZENYE MADHARA ZALETA ATHARI KWA WANAWAKE MKOANI MARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAMADUNI ZENYE MADHARA ZALETA ATHARI KWA WANAWAKE MKOANI MARA

Na Anthony Ishengoma-Mara.Jamii mkoani Mara bado inaendeleza mila potofu ya kuamini kuwa mwanamke asiyekeketwa ni mkosi kwa familia jambo ambalo linaendeleza vitendo vya kwa ukatili wa hali ya juu dhidi ya wanawake Mkoani humo.
Akiongea wakati wa ufanguzi wa Kikao kazi cha uzinduzi wa Kampeini ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto   leo Mkoani Mara Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Karolina Mtaphula amesema inapotokea binti anayekeketwa akapoteza maisha kutokana na ukeketaji binti huyo amekuwa akitupwa polini bila kuzikwa kwa taratibu za kawaida kwasababu jamii pia inaamini ni mkosi kwa jamii na kwa familia yake.
Aidha Mtapula aliongeza kuwa Jamii ya Mkoa wa Mara inatakiwa ijilinganishe na mikoa mingine ambayo haina mila ya ukeketaji ili kujenga ufahamu kuwa wanawake kutoka jamii hizo kama wamekuwa wakileta mikosi katika familia zao kama amabavyo mila zao inawafanya waamini.
‘’Wanawake katika Mikoa ambayo haina ukeketaji wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo na kufaidika kiel... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More