TAMASHA KUBWA LA UTALII KUFANYIKA ZANZIBAR, KUPAMBWA NA VIONGOZI WA KITAIFA NA TUZO KABAMBE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAMASHA KUBWA LA UTALII KUFANYIKA ZANZIBAR, KUPAMBWA NA VIONGOZI WA KITAIFA NA TUZO KABAMBE

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
TAMASHA la kihistoria la utalii linatarajiwa kufanyika visiwani Zanzibar kuanzia Oktoba 17 hadi 19 mwaka huu katika hoteli ya Verde, Mtoni visiwani humo na hiyo ni katika mpango kazi wa kupunguza umaskini na kuendeleza sekta ya utalii visiwani humo.
Akizungumza na vyombo vya habari Waziri wa Habari, utalii na mambo ya kale wa Zanzibar Mh. Mahmoud Kombo amesema kuwa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuzindua tamasha hilo akiambatana na viongozi wengine wa kitaifa akiwemo aliyekuwa Rais wa Zanzibar Dr. Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassani, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri wa utalii na maliasili kutoka Tanzania bara Dkt. Hamis Kigwangalla.
Mahmod ameeleza kuwa tamasha hilo ni fursa na litawavutia wawekezaji, wamiliki wa hoteli na wamiliki wa kampuni za kitalii wazawa na wageni kwa kutangaza bidhaa zao za kitalii na amesema kuwa shughuli za kitalii zimechangia kwa asilimia kubw... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More