TAMASHA LA WASAFI FESTIVAL KUZINDULIWA RASMI NOVEMBA 24 MTWARA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAMASHA LA WASAFI FESTIVAL KUZINDULIWA RASMI NOVEMBA 24 MTWARA

Na Khadija Seif,Globu ya Jamii 
Msanii wa Bongofleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz ametangaza ramsi kuanza kwa tamasha la Wasafi Festival Novemba 24 mwaka huu. 
Tamasha hlo linalotarajiwa kufanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini litaanzia Mkoani Mtwara ikiwa ni mara ya kwanza toka kuanza kwa Tv na Redio.
Akizungumza na wadau pamoja na wanahabari Leo Jijini Dar es salaam, Diamond amesema kuwa tamasha la Wasafi Festival lina lengo la kutoa burudani nchini na nje ya nchi ili kutangaza mziki wa kitanzania zaidi na kufundisha jamii jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri. 
Diamond amesema kuwa, licha ya kutangaza mziki huo kwenye mikoa ambayo itapata kushuhudia burudani hiyo ni wataanzia tarehe 24 mwezi huu kwenye mkoa wa Mtwara katika viwanja vya Nangwanda na ikifatiwa na mkoa wa Iringa,Morogoro , Zanzibar na mikoa mingine na pamoja na nchi ya Kenya. 
Amefafanua zaidi katika kila Mkoa utakaotembelewa pia watapata fursa kwa kukarabati shule , Wanafunzi kupatiwa sare za ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More