TAMBWE AFUFUA MAKALI, AFUNGA MABAO YOTE YANGA SC YAICHAPA SINGIDA UNITED 2-0 TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAMBWE AFUFUA MAKALI, AFUNGA MABAO YOTE YANGA SC YAICHAPA SINGIDA UNITED 2-0 TAIFA

Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
TIMU ya Yanga SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United usiku huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Shujaa wa Yanga leo ni mshambuliaji wake mkongwe, Mrundi Amissi Joselyn Tambwe aliyefunga mabao yote hayo kipindi cha kwanza na sasa wana Jangwani hao wanafikisha pointi 12 baada ya kushinda mechi zao zote nne za mwanzo.
Tambwe ambaye karibu msimu wote uliopita hakucheza kwa sababu alikuwa anasumbuliwa na maumivu, alifunga bao la kwanza dakika ya 29 kwa kichwa akimalizia krosi ya kiungo Ibrahim Ajib Migomba waliyekuwa naye Simba SC kabla ya kuhamia Yanga kwa wakati tofauti.
Tambwe tena akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 45 kwa shuti kali kutoka umbali wa mita 12 baada ya pasi nzuri ya beki wa kushoto, Gardiel Michael Mbaga.

Amissi Tambwe (kushoto) akiwa na Matheo Anthony baada ya kufunga leo

Kipindi cha pili Singida United walibadilika na kuanza kuwashambuliaji Yanga SC hususan baada ya kumuin... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More