TAMISEMI yapokea magari mawili kutoka USAID Boresha Afya - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TAMISEMI yapokea magari mawili kutoka USAID Boresha Afya

Na Mathew KwembeWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amepokea magari mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 na kusema kuwa magari hayo yataongeza thamani katika juhudi za serikali za kuimarisha utoaji wa huduma bora za afya katika mikoa ya Lindi na Mtwara.Akiongea katika hafla ya makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania David Thompson aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa dhamira yake ya kuboresha viwango vya afya kwa watanzania wote.“Kupitia msaada huu, Serikali ya Marekani inaungana na Serikali ya Tanzania kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa watu wote, katika jamii za watu wa Lindi na Mtwara, mkazo zaidi ukiwa kwa wanawake na vijana,” alisema.Kabla ya kuyapokea magari hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) David Thompson, Waziri Jafo alisema kuwa anatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Marekani kupitia Mradi wa USAID Bores... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More