TANESCO IHARAKISHE KUFIKISHA UMEME BANDARI KAVU -MGALU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANESCO IHARAKISHE KUFIKISHA UMEME BANDARI KAVU -MGALU

 Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu alipowasili kutembelea mradi wa bandari kavu ,Kwala Kibaha Vijiji, Mkoani Pwani
 Meneja wa mradi wa bandari kavu mhandisi Raymond Kweka ,akitoa taarifa ya mradi wakati naibu waziri wa nishati Subira Mgalu hayupo pichani alipotembelea mradi huo.
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wakazi wa  kijiji cha Mperamumbi Kibaha Vijijini.Picha na Mwamvua Mwinyi.
NAIBU Waziri wa Nishati,Subira Mgalu ameliagiza shirika la umeme (TANESCO) kuharakisha kufikisha umeme katika mradi mkubwa wa Bandari Kavu ,Kwala Kibaha mkoani Pwani  na wasiwe sehemu ya kuchelewesha mradi huo wa kimkakati wa kitaifa. 
Aidha amesema ,serikali ipo kwenye mpango wa kumpata mkandarasi wa mradi mpya wa Peri Urban ambapo anatarajiwa  kuanza kazi Novemba mwaka huu katika mitaa na vitongoji 182 na zimetengwa sh. bilioni 86 kwa ajili ya kazi hiyo. 
Akizungumza mara baada ya kutembelea ujenzi wa Bandari Kavu na kuongea na wakazi wa Mperamumbi, Kwala na Msua alitaka nishati... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More