TANESCO YAWASHA KITUO KIPYA CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME MADABA MKOANI RUVUMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANESCO YAWASHA KITUO KIPYA CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME MADABA MKOANI RUVUMA

HISTORIA imeandikwa upya kwa wakazi wa mji wa Songea na viunga vyake, baada ya serikali kupitia Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuwasha kituo kipya cha kupoza na kusambaza umeme wa kilovolti 220/33kv cha madaba usiku wa kuamkia Septemba 13, 2018. Kituo hicho ni sehemu ya vituo vipya vitano vilivyojengwa chini ya mradi wa umeme Makambaka- Songea.  Kwa wakazi wa Manispaa ya mji wa Songea ambao walitegemea umeme unaozalishwa kwa mashine za Jenereta, sasa wameunganishwa moja kwa moja kwenye Gridi ya Taifa, na mashine hizo zimezimwa rasmi.  Akizungumza mwanzoni mwa utekelezaji wa Mradi huo Oktoba 10, 2017, Meneja Mradi, Mhandisi Didas Lyamuya alisema, Mradi wa Makambako-Songea umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya kupoza na kusambaza umeme, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa kituo cha kupoza umeme cha Makambako. Lakini pia Ujenzi wa njia kuu ya usafirishaji Umeme wa kilovoti 220 yenye urefu wa kilometa 245 kutoka Makambako hadi Songea kupitia Madaba... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More