TANGA UWASA YANUFAIKA NA RUZUKU YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANGA UWASA YANUFAIKA NA RUZUKU YA ZAIDI YA BILIONI 1.2

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imenufaika na ruzuku ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.2 baada ya kutimiza masharti ya mkopo wa zaidi ya shilingi Bilioni 3 toka katika benki ya CRDB ya utekelezaji wa huduma ya Maji safi Jijini Tanga.
Ruzuku hiyo hutolewa na Benki ya watu wa Ujerumani (KFW) kutokana na Mamlaka husika kutimiza vema masharti ya mkopo huo ikiwa pamoja na zoezi zima la marejesho huku likizingatiwa suala la utekelzaji wa mradi uliopewa fedha hizo.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya ugeni kutoka KFW ya nchini Ujerumani kutembelea mradi wa maboresho ya huduma ya maji safi Jijini Tanga.
Alisema mkopo huo umewasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa maji hasa katika maeneo yaliyokuwa na mgawo wa maji bila sababu yaliyochangiwa na udogo wa vipenyo vya mabomba yaliyokuwa yanapeleka maji kwenye maeneo hayo.“Kama nilivyoonyesha kwamba tume... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More