TANGAZO KWA UMMA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANGAZO KWA UMMATAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuukumbusha Ummakwamba wale wote wanaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti na nyaraka mbalimbali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:


(1)  Huduma hizo zinatolewa katika Ofisi za Wizara Mjini DODOMA jengo la LAPF, Barabara ya Makole Ghorofa la 6.


(2) Malipo ya nyaraka zitakazothibitishwa yatalipwa kwa njia ya benki, akaunti namba 0150275408200 Foreign Collection Account, CRDB Bank kwa kiasi cha Shilingi Elfu Kumi na Tano tu kwa kila nyaraka (@TSHS 15,000/=). Hati ya malipo ya benki iwasilishwe Wizarani ili kuthibitisha malipo hayo.


(3) Mteja mwenye nyaraka yeyote inayohusu masuala ya talaka, ndoa, hali ya ndoa, tangazo la kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Kifo, cheti cha ndoa anatakiwa kuanzia ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration, Insolvency, Trusteeship Agency- RITA) Dar es Salaam.


(4) Vyeti vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishw... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More