“Tangu Nimeoa Mabinti Wamepunguza Usumbufu”- Ali Kiba - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

“Tangu Nimeoa Mabinti Wamepunguza Usumbufu”- Ali Kiba

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa tangu ameoa Miezi michache iliyopita anaona mabadiliko makubwa kwani mabinti wamekuwa hawamsumbui kama alivyokuwa single.


Kama ilivyo kwa wasanii wengi maarufu ni kawaida kwa warembo kujigonga kwao kutokana na labda umaarufu au hata pesa ambazo wanakuwa nazo na Ali Kiba aliwahi kukiri kukutana na changamoto kama hizo.


Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Al Kiba amefunguka kuwa tangu amefunga ndoa amebadili tabia yake na kwa saaa anamuheshimu sana Mke wake.


Lakini pia Kiba amekiri kuwa usumbufu  aliokuwa anaupata kutoka kwa mabinti ambao walikuwa wanamtongoza umepungua kabisa kwa sababu wanajua hivi sasa ameoa.


Ali Kiba ameweka wazi hata kwa upande wake binafsi amebadilika kwani amekuwa akijiheshimu na kumuheshimu Mke wake tofauti na  alivyokuwa kabla hajaoa ambapo wasichana walikuwa wanamsumbua wakijua ya kwamba labda wanaweza  kupata nafasi ya wao Kuolewa kitu ambacho kwa sasa hakipo kabi... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More