Tanzania, DRC Zaanza Mazungumzo Ujenzi wa Kinu/Kiwanda cha Kuchenjua Colbat - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania, DRC Zaanza Mazungumzo Ujenzi wa Kinu/Kiwanda cha Kuchenjua ColbatAsteria Muhozya na Rhoda James, GEITA.
 Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini imeanza kufanya mazungumzo na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili iweze kujenga Kiwanda cha Kuchenjua madini ya Colbat nchini. Hayo yalibainishwa Oktoba 19, mkoani Geita  na Waziri wa Madini wa Tanzania Angellah Kairuki wakati wa kuhitimisha ziara ya siku Nne ya  Waziri wa Madini wa Kongo (DRC), Martin Kabwelulu aliyoifanya nchini kwa mwaliko wa Waziri Kairuki.
Kairuki alisema kuwa, nchi ya Kongo ndiyo mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat duniani ambapo asilimia 70 ya madini hayo duniani yanazalishwa nchini humo.Aliongeza kuwa, kwa sasa nchi hiyo inayo changamoto ya kusafirisha madini hayo yakiwa ghafi ikiwemo ukosefu wa umeme wa kutosheleza kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hivyo.
“Tumekubaliana kuendelea na mazungumzo  na Kongo ili shughuli za uchenjuaji na uyeyushaji wa madini hayo ufanyike nchini  kwa kuwa tumeshaanza kuwekeza kwenye Vinu/v... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More