Tanzania kuwa kitovu cha kuzalisha chakula Afrika. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania kuwa kitovu cha kuzalisha chakula Afrika.

Serikali ya Ufaransa kupitia Balozi yake nchini Tanzania imeahidi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA na wadau wengine kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha uzalishaji wa chakula na malighafi zingine katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. 
Hayo yamesemwa na Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Mhe. Balozi Fredrick Clavier wakati wa ziara yake chuoni hapo iliyolenga kujifunza kuhusu Mradi wa Kilimo Hifadhi unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ufaransa kwa kushirikiana na Shirika la Misaa la Switzerland (SWISSAID) na kutekelezwa na timu ya watafiti wa SUA, SAT na TOAM ambapo Ubalozi huo umechangia kiasi cha EURO 850,000. 
“Mradi huu ni wa miaka mitano unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wapatao 6000 na kuhifadhi bayoanuai na mazingira kupitia uzalishaji kwa kutumia kilimo hai, matumizi sahihi ya mnyororo wa thamani wa kilimo hai, kuimarisha vikundi 269 vya wakulima wadogowadogo taasisi mwamvuli za vyama hivyo na kuweka kumbukumbu mbinu za kilimo hai zilizokubaliwa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More