TANZANIA KUWAKILISHWA NA WAOGELEAJI WANNE KWENYE MASHINDANO YA DUNIA NCHINI CHINA DESEMBA 11 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANIA KUWAKILISHWA NA WAOGELEAJI WANNE KWENYE MASHINDANO YA DUNIA NCHINI CHINA DESEMBA 11

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TANZANIA itawakilishwa na waogeleaji wanne katika mashindano ya dunia ya kuogelea yaliyopangwa kufanyika nchini China kuanzia Desemba 11 mpaka 16 eneo la Hangzhou Olympic and International Expo Center.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Asmah Hilal aliwataja waogeleaji hao kuwa ni Kalya Temba na Celina Itatiro kwa upande wa wanawake na Collins Saliboko na Hilal Hilal watawakilisha upande wa wanaume.
Asmah alisema kuwa kocha maarufu nchini, Alexander Mwaipasi na Mwenyekiti wa chama chao, Imani Dominick wataambatana na timu hiyo nchini China.

Waogeleaji wa Tanzania, Celina Itatiro (wanne kutoka kushoto) na Kayla Temba (wa tatu kutoka kulia) katika picha ya pamoja na uongozi Chama cha kuogelea na nchini (TSA) na wazazi mara baada ya kuondoka jana kwenda Hangzhou, China kushiriki mashindano ya Dunia. Katikati ni kocha wa timu hiyo, Alexander Mwaipasi.  

Alisema kuwa Kayla na Celina wameondoka jana usiku wakati Collins ataungana na wenzake mj... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More