Tanzania kuwakilishwa na waogeleaji wanne Mashindano ya Dunia China - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania kuwakilishwa na waogeleaji wanne Mashindano ya Dunia China

Tanzania itawakilishwa na waogeleaji wanne katika mashindano ya dunia ya kuogelea yaliyopangwa kufanyika nchini China kuanzia Desemba 11 mpaka 16 eneo la Hangzhou Olympic and International Expo Center. Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea nchini (TSA), Asmah Hilal aliwataja waogeleaji hao kuwa ni Kalya Temba na Celina Itatiro kwa upande wa wanawake na Collins Saliboko na Hilal Hilal watawakilisha upande wa wanaume.
Asmah alisema kuwa kocha maarufu nchini, Alexander Mwaipasi na Mwenyekiti wa chama chao, Imani Dominick wataambatana na timu hiyo nchini China. Alisema kuwa Kayla na Celina wameondoka jana usiku wakati Collins ataungana na wenzake mjini Hangzhou akitokea Uingereza na Hilal atakenda China akitokea Dubai.
Alisema kuwa waogeleaji hao wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo ambayo pia yataambatana na mkutano mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa kuogelea duniani (Fina) na kozi ya makocha, Mkutano Mkuu wa Fina na kozi ya makocha utaanzia kesho.  “ Ni matarajio yetu kuwa wat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More