Tanzania kuwakillishwa na waogeleaji wanne mashindano ya Dunia - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania kuwakillishwa na waogeleaji wanne mashindano ya Dunia

Chama Cha mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kimetangaza majina ya waogeleaji wanne ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika katika mji wa Gwangju, Korea Kusini.
Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro amewataja waogeleaji hao ni Hilal Hemed Hilal na Collins Saliboko ambao watashindana kwa upande wa wanaume ambapo kwa upande wa wasichana ni Sylvia Caloiaro na Shivani Bhatt.
Waogeleaji hao kwa sasa wapo katika maandalizi makali kwa ajili ya mashindano hayo yaliyopangwa kuanza Julai 18 mpaka 29.
Hilal kwa sasa anafanya mazoezi Dubai kufuatia udhamini wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fina), nchini Dubai na Collins anajifua shuleni kwake, St Felix Uingereza huku Sylvia na Shivani wanatoka klabu ya Taliss-IST wanafanya mazoezi hapa hapa nchini.
Katibu Mkuu wa TSA, Inviolata Itatiro alisema kuwa aaogeleaji hao wamepata nafasi hiyo baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa.
Inviolata alisema kuwa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (Fin... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More