TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO

Na. Jeshi la Polisi.

Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) imemalizika Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la Polisi nchini likishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza imeenda Kenya na ya tatu Uganda.

Polisi Tanzania imeshika nafasi hiyo baada ya kuchukua jumla ya Medali 64, 15 za dhahabu, 25 za fedha na 24 za shaba huku Kenya ikiwa na medali 68, 25 dhahabu , fedha 20 na shaba 24.

Mshindi wa Tatu Uganda alijinyakulia Medali 36, Rwanda 27, Burundi nane, Sudani Kusini sita na Sudani moja ambapo timu za Polisi Tanzania zimetwaa ubingwa katika Soka, Mpira wa pete, Judo, na Kulenga Shabaha kwa upande wa Wanaume.

Akifunga Michezo hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Wanamichezo hao kudumisha umoja na Amani katika mataifa wanayotoka ikiwemo kutumia michezo hiyo kubadilishana mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu.

Aliwapongeza Wanamichezo wote walioshiriki michezo hiyo kwa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More