TANZANIA YAITOA BURUNDI KWA MATUTA NA KUSONGA MBELE KUFUZU KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANIA YAITOA BURUNDI KWA MATUTA NA KUSONGA MBELE KUFUZU KOMBE LA DUNIA QATAR 2022

Na Saada Salim, DAR ES SALAAM
TANZANIA imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kwa ushindi wa penalti 3-0 kufuatia sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Sare ya 1-1 yalikuwa marudio ya matokeo ya mchezo wa kwanza Uwanja wa Intwari mjini Bujumbura na kufanya sare ya jumla ya 2-2 kabla ya kipa mzoefu, Juma Kaseja Juma kwenda kuibuka shujaa kwenye mikwaju ya penalti.
Beki mkongwe anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni alianzisha biashara nzuri kwa Taifa Stars baada ya kufunga penalti ya kwanza na wenzake, kiungo Himid Mao Mkami ‘Ninja’ na beki Gardiel Michael Mbaga wakafunga pia.
Kaseja aliwakata maini Warundi baada ya kuokoa penalti ya kwanza ya Int’hamba Murugamba iliyopigwa na mtokea benchi, Omar Ngandu aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Kanakimana Bienvenu Kanakimana dakika ya 67 na haikuwa ajabu Saido Berahino na Bigirmana Gael wakapiga nje mfululizo. 
Katika dakika 90 za mchezo,... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More