Tanzania yakabiliwa na upungufu wa samaki tani 350,000 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania yakabiliwa na upungufu wa samaki tani 350,000

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
Tanzania ina Upungufu wa Tani zipatazo 350,000 za Samaki kwa mwaka huku mahitaji yakiwa ni Tani 700,000 ambapo kwa mwaka kiasi cha tani 350,000 kinazalishwa,hivyo watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya uzalishaji ili kufikia malengo ya mahitaji ya samaki.
Kauli hiyo imeelezwa jijini Arusha na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega wakati wa kutiliana saini makubaliano ya mashirikiano baina ya serikali ya Tanzania na nchi ya Uholanzi katika Nyanja za maendeleo ya ufugaji wa Samaki na Kuku.
Ulega amesema kuwa ushirikiano huo wa kimaendeleo na nchi ya Uholanzi umefikia miaka zaidi ya 40 katika njanja mbali mbali,ikiwemo kilimo cha Mboga mboga,Viazi Mviringo, Ufugaji wa kuku na Samaki yanayosaidia kuongeza uzalishaji wa protini na mapato kwa Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Tanzania inauhitaji mkubwa wa protini inayotokana na samaki na kuku ndio maana wamekubaliana na Taifa hilo la uholanzi kuweza kuboresha Nyanja hizo kwa lengo la kutoa elimu ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More