TANZANIA YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA UTALII SEOUL, KOREA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANIA YANG’ARA KATIKA MAONYESHO YA UTALII SEOUL, KOREA

Ubalozi wa Tanzania Seoul, kwa kushirikiana na wadau wa Utalii kutoka sekta binafsi wameshiriki katika maonyesho makubwa ya Kimataifa ya “Seoul International Tourism Industry Fair” yaliyofanyika jijini Seoul kuanzia Juni 6-9, 2019 na kuandaliwa na Korea World Travel Fair (KOTFA) kwa kushirikiana na Seoul International Travel Mart (Seoul Metropolitan City). Maonyesho hayo makubwa na ya aina yake yalijumuisha wadau kutoka nchi mbalimbali za Asia, Ulaya, America, Africa na Middle East wakiwemo:  Tour Operators, Travel Fairs, wamiliki wa Hoteli na Migahawa (Restaurants), Media, na wamiliki wa vyombo vya usafiri (Ndege, Cruise ships). Tanzania iliwakilishwa na Ubalozi wa Tanzania Korea Kusini, Kampuni ya Utalii Eastenders, Zara Tours, Travel Booking Guide kwa kupitia Mwakilishi wake aliye Korea, Ms. Han Bitnarae, na SAFANTA Tours & Travel ya Zanzibar.Kwa ujumla maonyesho hayo yalifana sana kwa Makampuni hayo kupata wenzao wa kushirikiana nao kibiashara kupitia B2B, kubadilishana uzoefu... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More