TANZANIA YAPIGA HATUA UWEZESHAJI WANAWAKE - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANIA YAPIGA HATUA UWEZESHAJI WANAWAKE

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Kushoto) akiwa katika katika Mkutano Mkuu wa 63 Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea katika jiji la New York nchini Marekani.
Na Mwandishi Wetu – New York Marekani.
Tanzania ni nchi mmojawapo duniani iliyofanikiwa kupiga hatua katika kuwawezesha wanawake kijikwamua kiuchumi kwa kuwasaidia kupata mikopo isiyo na riba inayowawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo na Mh Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea New York, Marekani.
Waziri Ummy alieleza kuwa Tanzania imepiga hatua katika uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za mikopo na kufanyia marekebisho Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 2018 ambayo imefuta Riba kwa mikopo yote inayotolewa kwa wanawake kupitia Halmashauri.
Alisema Halmashauri zimekuwa zikichangia asilimia 5 ya mapato y... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More