Tanzania yashiriki katika mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzania yashiriki katika mkutano wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
Katibu Mtendaji wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Stergomena Tax, akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa  Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Council of Ministers),  unaofanyika Windhoek, Namibia, kuanzia tarehe 15 -17 Machi, 2019.  Mkutano huu, unahudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mawaziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mawaziri wa Fedha pamoja nchi 16 wanachama wa SADC ambapo Tanzania inawakilishwa katika mkutano huu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.);  Waziri wa Viwanda na  Biashara, Mhe. George Kakunda (Mb.); na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.). 
Masuala yanayojadiliwa katika mkutano huu ni pamoja na  Taarifa ya Utekelezaji wa mipango na mikakati ya SADC; Taarifa ya Kamati ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Kamati ya Usimamizi wa Rasilimali watu; Hatua zilizofikiwa katika mchakato wa Visiwa vya Komoro kujiunga na SADC n... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More