TANZANITE YAWAPIGA ZAMBIA 2-1 NA KUTWAA KOMBE LA COSAFA U20 WANAWAKE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZANITE YAWAPIGA ZAMBIA 2-1 NA KUTWAA KOMBE LA COSAFA U20 WANAWAKE

Na Mwandishi Wetu, PORT ELIZABETH 
TIMU ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Zambia leo Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth. 
Mabao ya Tanzania inayofundishwa na kocha Bakari Nyundo Shime anayesaidiwa na Edna Lema yamefungwa na Opa Clement dakika ya 24 na Protasia Mbunde dakika ya 87.
Ushindi huo pia ni sawa na kulipa kisasi kwa Tanzanite baada ya kufungwa mabao 2-1 pia na Zambia katika mchezo wa awali, kwenye Kundi B.
Ikumbukwe Tanzania iliingia fainali baada ya kuwafunga wenyeji, Afrika Kusini Uwanja wa Uwanja wa Gelvandale mjini Port Elizabeth.

Mechi nyingine za Kundi B, Tanzania ilishinda 2-0 dhidi ya Botswana na 8-0 dhidi ya Eswatini.... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More