TANZIA: Bingwa wa Dunia wa mbio za mita 400, Nicholas Bett afariki dunia - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZIA: Bingwa wa Dunia wa mbio za mita 400, Nicholas Bett afariki dunia

Bingwa wa Dunia wazamani wa mbio za mita 400, Nicholas Bett amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea hii leo siku ya Jumatano majira ya asubuhi huko Nandi.Kamanda wa polisi wa County ya Nandi nchini Kenya, Patrick Wambani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo hii leo majira ya asubuhi.Bett amekuwa mwanariadha wakwanza kutoka Kenya kushinda ubingwa wa Dunia kwakutumia muda wa dakika 47 na sekunde 79 kwenyemichuano ya iliyofanyika Beijing nchini China mwaka 2015.Deeply saddened by the death of former 400m hurdles World Champion Nicholas Bett who died today in a tragic road accident. Bett earned the country great honours in his outstanding victories. My deepest sympathies and heartfelt condolences to his family, relatives and friends. pic.twitter.com/9Xgqt1tFr3


— Uhuru Kenyatta (@UKenyatta) August 8, 2018Lakini pia mwanariadha huyo wa Kenya aliwahi kuvunja rekodi ya dunia katika kukimbiza upepo baada ya kutumia dakika 48 na sekunde 24.


Nicholas Bett akiwa amezaliwa Januari 27, 1990 ni mtoto wa pili kwenye familia yao yenye watoto watatu. Kaka yake Haron Koech akiwa kwenye timu ya taifa ya Kenya ya Olympics huku marehemu akiwa ameacha mke na watoto watatu.


The post TANZIA: Bingwa wa Dunia wa mbio za mita 400, Nicholas Bett afariki dunia appeared first on Bongo5.com.


Source: Bongo5Read More