TANZIA: Muigizaji mkongwe wa kundi la Kaole, Ramadhani Mrisho maarufu kama Mashaka afariki dunia - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZIA: Muigizaji mkongwe wa kundi la Kaole, Ramadhani Mrisho maarufu kama Mashaka afariki dunia

Aliyewahi kuwa msanii wa maigizo wa kundi la Sanaa la Kaole, Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama ‘Mashaka’ amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo asubuhi Jumamosi, Oktoba 20, 2018.Abdallah Ditopile ambaye ni mtoto wa marehemu amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema baba yake aliugua ghafla usiku ndipo wakamkimbiza hospitali kwa ajili ya matibabu na Ilipofika asubuhi hali yake ikabadilika, madaktari walitupatia rufaa ya kumpelekea katika Hospitali ya Muhimbili Tawi la Mloganzila, wakati tukijiandaa kuita ambulance, akakata roho, baba ametutoka katika hospitali ya Amana jijini Dar es salaam.


Mashaka alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Presha pamoja na kisukari ambapo jana alizidiwa gafla na kukimbizwa hospitali ya Amana, madaktari walifanikiwa kumpa huduma ya kwanza na matibabu ikiwa pamoja na kumuwekea mashine ya kupumulia ya oksijeni.


”Kwa sasa ndugu wamekusanyika nyumbani kwa kaka mkubwa wa marehemu, maeneo ya Ilala Sokon... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More