Tanzia- Mzee Majuto Afariki Dunia - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Tanzia- Mzee Majuto Afariki Dunia

Msanii mkongwe wa Bongo movie aliyejizolea umaarufu kwa vichekesho vyake amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.


Mzee Majuto amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Muhimbil baada ya kulazwa kwa siku kadhaa tangu wiki chache zilizopita baada ya kuugua.


Taarifa za msiba kwa mara ya kwanza zilitolewa na mchekeshaji Joti Kupitia ukurasa wake wa Instagram:


“R.I.P @Kingmajuto Umetuachia Maumivu Makubwa sana ktk Tasnia ya Comedy Tanzania Sisi wanao,Tutakukumbuka kwa kazi zako,Upendo wako,Tabasamu lako Daima milele,Tulikupenda sana ila Mungu amekupenda zaidi,Pumzika kwa Amani Mzee wetu”.


Mzee Majuto alianza kuugua mwaka jana na mwaka huu serikali kwa kushirikana na wananchi walichanga pesa na kumpelekeka kwenye matibabu nchini India.


The post Tanzia- Mzee Majuto Afariki Dunia appeared first on Ghafla!Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More