TANZIA: Professor Jay afiwa na Baba yake mzazi (+audio) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TANZIA: Professor Jay afiwa na Baba yake mzazi (+audio)

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule a.k.a Professor Jay amefiwa na baba yake mchana wa leo Septemba 7, 2018 katika Hospitali ya St. Kizito .Professor Jay akizungumza na Bongo5 amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na Presha, ambapo amedai leo asubuhi baba yake aliamka akiwa na afya njema lakini akiwa njiani kwenye gari alizidiwa na ndipo lilipokuja wazo la kumpeleka Muhimbili kwa Madaktari wake.


Professor amesema kabla ya kupelekwa Muhimbili alihityaji wafanye sala kwanza na alipomaliza kusali sala ya salamu Maria, akaaga dunia.


Hata hivyo, Professor Jay amesema kwa sasa yupo njiani akitokea Dodoma kwenye vikao vya bunge na ameahidi kutoa ratiba rasmi za mazishi baada ya kukutana na ndugu.


Bongo5 Media Group inatoa pole kwa familia ya Mhe. Joseph Haule.


The post TANZIA: Professor Jay afiwa na Baba yake mzazi (+audio) appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More