Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Taratibu Mpya za Kusimamia Uagizaji wa Sukari Kukamilika Oktoba - Mwijage

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZOSerikali imepanga kukamilisha utaratibu mpya wa kuagiza sukari nchini ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu. Utaratibu huo mpya unatagemewa kuwa mwarobaini wa kukomesha mrundikano wa sukari kwenye viwanda vya sukari nchini.
Hakikisho hilo limetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mheshimiwa Charles Mwijage wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya sukari nchini.
Waziri Mwijage ameliambia bunge kuwa sukari inayozalishwa nchini haikidhi mahitaji na kwa mwaka 2018/19 uzalishaji unakadiriwa kufikia tani 353,651 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na hakuna kiwanda kinachozalisha sukari kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
Upungufu huo wa sukari inayozalishwa nchini umesababisha nakisi ya sukari takribani tani 316,349,  tani 161,349 zikiwa za matumizi ya kawaida na tani 155,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani.
"Hadi kufikia Septemba 5, 2018, viwanda vyetu vilizalisha jumla ya tani 119,671.19 ambazo ni sawa na asilimia 33.84 ya malengo ya uzalisha... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More