TARIMBA ABBAS MWENYEKITI KAMATI YA USAJILI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

TARIMBA ABBAS MWENYEKITI KAMATI YA USAJILI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam umemteua Tarimba Abbas kuwa mwenyekiti  odi ya   wa kamati maalumu ya kushughulikia usajili na mikataba ya wachezaji akisaidiwa na aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecky Saddick.
Uteuzi huo umefanywa na bodi ya wadhamini na kuamua kuunda  kamati maalumu kwa ajili ya kushughulikia usajili na mikataba yote ya wachezajia.
Kamati hiyo maalumu inaanza kazi moja kwa moja kuhakikisha wanafanya usajili wa makini na pia kuipitia mikataba ya wachezaji waliomaliza muda wao na wale waliopo bado hawajamaliza.
Bodi ya wadhamini imeweza pia kuteua wajumbe watakaosaidiana ambao ni  Abdallah bin Kleib, Ridhiwani Kikwete,Nyika Hussein,Samuel Lukumay,Mashauri  Lucas, Yusuphed Mhandeni na Ahmed Islam.
Wengine ni Makaga Yanga,Majid Suleiman na Ndama ambao wanatakiwa kuhakikisha usajili wa Yanga unaenda kama walivyopanga.
Mkutano huo uliweza kumalizika kwa amani na wanachama wote kuazimia kwenda kat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More